1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington: Polisi wasema watu wanne pekee ndio waliofariki kwenye ajali ya daraja.

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcm

Polisi wa jimbo la Minnesota nchini Marekani wamesema ni watu wanne pekee waliothibitishwa kwamba wamefariki kutokana na ajali ya kuporomoka daraja linalovuka mto Mississippi mjini Minneapolis.

Idadi hiyo ni tofauti na idadi ya watu kiasi tisa iliyokuwa imetangazwa hapo awali.

Hata hivyo maafisa wa serikali wanasema idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa kuwa makundi ya wakoaji yangali yakitafuta maiti au watu walionusurika kwenye ajali hiyo.

Taarifa za awali zilisema magari kati ya hamsini na mia moja yalikuwa kwenye daraja hilo

Polisi wamesema sababu za ajali hiyo hazijajulikana, ingawa wamekanusha uwezekano wa ajali hiyo kuwa imesababishwa na vitendo vya kigaidi.