1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rais Bush kulihutubia taifa

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYU

Rais George W Bush wa Marekani anatarajiwa kulihutubia taifa leo usiku katika bunge linalodhibitiwa na chama cha Democratic. Rais Bush anataraji kutoa maelezo kuhusu sera yake kuelekea Irak ambayo imekosolewa vikali na wabunge.

Hapo awali naibu kiongozi wa kundi la al-Qaeda Ayman al-Zawahiri amemkejeli rais Bush juu ya mpango wake wa kuongeza idadi ya wanajeshi nchini Irak. Kwenye ukanda wa video uliotolewa na kundi la al-Qaeda, al Zawahiri amemtaka rais Bush atume jeshi lote la Marekani nchini Irak akisema majeshi kumi ya aina hiyo yatashindwa nchini Irak.

Mapema mwezi huu rais Bush alitangaza ataongeza wanajeshi zaidi ya 20,000 nchini Irak.