1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Seneta Obama ajiandaa kwa kampeni ya uchaguzi

17 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCa8

Nchini Marekani,Seneta wa chama cha Demokrats,Barack Obama amechukua hatua yake ya kwanza kuelekea kwenye kampeni ya uchaguzi wa rais,kwa kutoa ombi la kuundwa kamati itakayoanza kukusanya michango.Obama mwenye umri wa miaka 45, ambae baba yake ni Mkenya na mama ni Mmarekani mweupe,anatazamiwa kutoa changa moto kali katika kampeni ambayo hadi hivi sasa imedhibitiwa na Seneta wa New York,Bibi Hillary Clinton.Obama, anatazamiwa kutoa tangazo rasmi la uamuzi wake tarehe 10 mwezi wa Februari huko Illinois,ambalo ni eneo analoliwakilisha katika Seneti.