1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Uamuzi wa rais Bush kubatilisha hukumu dhidi ya Libby wakosolewa vikali

3 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmP

Wabunge wa chama cha Democratic nchini Marekani wamelaani vikali hatua ya rais George W Bush kubatilisha hukumu dhidi ya afisa wa zamani wa ikulu ya white house, Lewis ´Scooter´ Libby.

Rais Bush amebatilisha hukumu ya kifungo cha miaka 30 garezani dhidi ya Libby baada ya kupatikana na makosa ya kuwadanganya wachunguzi wa serikali kuhusu kesi iliyochunguza ikiwa maafisa wa ikulu ya Marekani walifichua jina la afisa wa ujasusi, Valerie Plame, mnamo mwezi Julai mwaka wa 2003.

Kiongozi wa chama cha Democrats katika bunge la Marekani, Nancy Pelosi, amesema uamuzi wa rais Bush si wa haki, unaruhusu uhalifu, na unasaliti imani ya Wamarekani.

Mbunge wa chama cha Democratic, Harry Reid, kwa upande wake amesema uamuzi wa rais Bush ni aibu. Adha mbunge huyo amesema katiba ya Marekani inampa rais Bush mamlaka ya kubatilisha hukumu lakini historia itamhukumu kwa kutumia mamlaka yake vibaya kumpendelea Lewis Libby aliyepatikana na makosa ya kuvunja sheria.

Akitangaza uamuzi wake rais Bush alisema anaheshimu uamuzi wa mahakama lakini akasema hukumu dhidi ya Libby imevuka mpaka. Makamu wa rais wa Marekani, Dick Cheney, ameunga mkono uamuzi huov wa rais Bush.

Kesi dhidi ya Lewis ´Scooter´ Libby itachunguzwa upya.