1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Uturuki yaonywa kutoingia Iraq

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7H2

Marekani imeitahadharisha Uturuki dhidi ya kutuma vikosi kaskazini mwa Iraq kuwaandama waasi wa Kikurdish.

Onyo hilo limekuja baada ya waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayep Erdogan kuidhinisha kuchukuliwa kwa hatua za kijeshi dhidi ya waasi kutoka chama cha Wafanyakazi wa Kikurdistan PKK nchini Iraq.Wanajeshi 15 wa Uturuki wameuwawa katika mashambulizi ya chama cha PKK katika kipindi cha siku tatu zilizopita.

Uturuki inaamini waasi hao wamekuwa wakijificha kwenye eneo la Wakurdish kaskazini mwa Iraq ambapo wana uhuru wa kujipatia silaha na mabomu.