1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Bush kesho kutangaza siasa zake mpya huko Iraq

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcE

Rais George Bush wa Marekani kesho anatarajiwa kutangaza mipango mbadala katika siasa zake nchini Iraq.

Hata hivyi hakuna taarifa zaidi kutoka Ikulu ya Marekani, lakini imekuwa ikihisiwa kuwa Rais Bush anataka kuongeza askari 20,000 nchini Iraq.

Spika mpya wa bunge la Congress la Marekani, Nancy Pelosi anayetoka chama cha Democrat, alionya kuwa bunge hilo halitopitisha maombi yoyote ya fedha kwa ajili ya kuongeza askari huko Iraq.

Wakati huo huo, Ikulu ya Marekani imesema kuwa Rais Bush atamteua balozi wa sasa wa Marekani nchini Iraq, Zalmay Kahlilzad kuwa balozi mpya wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.

Nchini Iraq, Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi UNHCR limeomba msaada wa dola milioni 60 kwa ajili ya wakimbizi zaidi ya milioni 1 na laki saba nchini Iraq.

Shirika hilo linakadiria kuwa kati wairaq elfu 40 hadi elfu 50 wanakimbia maeneo yao kila mwezi kutokana na mauaji yanayoendelea nchini humo.

.