1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Democratic leo yaanza kudhibiti bunge la nchini Marekani

4 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdL

Chama cha Demokratic leo kinatazamiwa kuchukua rasmi udhibiti wa baraza la congress la Marekani ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 12 iliyopita.

Chama hicho kinatarajiwa kumchagiza Rais George Bush kubadilisha uelekeo wake katika vita ya Iraq, mnamo wakati ambapo Rais Bush amesema kuwa anatarajia kufanya mabadiliko makubwa katika mikakati yake ya kijeshi nchini Iraq.

Chama cha Democratic kilipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa maseneta hivi karibuni.

Seneta wa jimbo la Carlfonia Nancy Pelosi anatarajiwa kuwa mwanamke wa kwanza kukamata nafasi ya juu ya uspika katika bunge la Congress la Marekani.