1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Mawaziri Iraq wapitisha muswaada utakaofungua njia ya kushtaki makampuni ya usalama ya Kigeni yatakapokosea

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BE

Wizara za ulinzi na mambo ya nje nchini Marekani zimekubaliana kuimarisha sheria zinazosimamia mashirika ya kibinafsi ya usalama nchini Iraq.Mabadiliko yaliyopendekezwa katika sheria hizo yamekuja kufuatia tukio la hivi karibuni lililowahusisha walinzi wa usalama kutoka kampuni ya Marekani ya Black Water katika mauaji ya raia 17 wa Iraq .Kampuni hiyo ilisema walinzi wake walichukua hatua hiyo kwa kuzingatia sheria.Wakati huohuo baraza la mawaziri nchini Iraq limeidhinisha muswaada wa sheria ambao unaondoa kinga kwa mashirika ya kigeni yanayoendesha shughuli zake nchini humo. Kwa mujibu wa Muswada huo wa sheria unaosubiri kuidhinishwa na bunge makampuni ya kigeni ya usalama nchini Iraq yatashtakiwa endapo yanatenda kosa lolote nchini humo.

Muswaada huo unabatilisha amri iliyotolewa mwaka 2004 na aliyekuwa wakati huo kiongozi mkuu wa jeshi la Marekani nchini Iraq Paul Bremer.Sheria hiyo iliyapa mashirika ya kigeni kinga dhidi ya kukabiliwa na mashtaka nchini Iraq.