1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Mswada wa ratiba ya majeshi nchini Iraq waangushwa

19 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhI

Chama cha Republican nchini Marekani kimezuia pendekezo la Chama cha Democrat kwenye bunge la Marekani la kumlazimu Rais Bush kuondoa sehemu kubwa ya majeshi ya marekani nchini Iraq ifikapo mwisho wa mwezi Aprili mwaka uajo.Chama cha Democrat hakikupata kura 60 zinazohitajika kuidhinisha mswada huo.Kura hiyo ilifanyika wakati bunge la marekani lilijadiliana usiku kucha kuhusu uvamizi wa Iraq.Rais Bush anasema kuwa atapiga kura ya turufu mswada wowote utakaomlazimu kuunda ratiba maalum ya kuondoa majeshi ya marekani nchini Iraq.