1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Wanajeshi kuondoka Irak kwa awamu

14 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPm

Rais George Bush kwa mara nyingine amekataa miito juu ya kuyaondoa majeshi yote ya Marekani kutoka nchini Irak lakini amesema kwamba wanajeshi 30,000 watarudishwa nyumbani hadi kufikia mwezi Julai mwaka ujao.

Kundi la kwanza la wanajeshi 5,700 litaondoka Irak wakati wa Krismasi ya mwaka huu.

Rais Bush amesema kuwa amekubali mapendekezo yaliyo wasilishwa na kamanda mkuu wa majeshi ya Marekani nchini Irak Jenerali David Petraeus.

Wajumbe wa chama chama cha Demokratik wanapinga mpango wa kuondoa majeshi hayo hatua kwa hatua, wajumbe hao wanasema kuwa Marekani haiwezi kuendelea kuweka majeshi yake nchini Irak.

Wakati huo huo Jamuhuri ya Georgia imethibitisha kuwa itapunguza kikosi cha wanajeshi wake 2000 kutoka nchini Irak hadi wanajeshi 300 kufikia msimu ujao wa kiangazi.