1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washukiwa wa al Qaeda wakamatwa

22 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cf5a

Maafisa wa usalama nchini Saudi Arabia wamelitia mbaroni kundi la wanamgambo wa al Qaeda wanaoshukiwa walikuwa na njama ya kufanya mashambuzili nchini humo wakati wa hija.

Hata hivyo maafisa wa Saudi Arabia wamesema washukiwa hao hawakutaka kupalenga mahala patakatifu zaidi katika dini ya kiislamu, Makkah, wala kuwalenga mahujaji, bali walitaka tu kusababisha mtafuruku na kuvuruga usalama.

Hakuna habari zilizotolewa kuhusu idadi ya wanamgambo waliokamatwa.