1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasichana wa Chibok waungana na wenzao

Sekione Kitojo
31 Mei 2017

Wasichana 82 walioachiliwa huru na kundi la Boko Haram sasa wanajiunga na wale waliokwishaachiliwa hapo kabla katika mpango wa kuwarejesha katika maisha ya kawaida, kwa mujibu wa serikali ya nchi hiyo. 

https://p.dw.com/p/2dvDw
Nigeria - Heimkehr der Chibok Mädchen
Picha: Reuters/A. Sotunde

Aisha Alhassan, waziri wa masuala ya wanawake na maendeleo ya kijamii, amesema jana  kwamba wanawake hao watahudhuria miezi kadhaa ya mafunzo kwa ajili ya kuwabadilisha. 

Ndani ya kipindi hicho, watakuwa na madaktari na wauguzi kuwasaidia kupona kutoka katika fadhaa ya miaka mitatu wakiwa katika maisha ya kutekwa nyara. 

Hata hivyo, kumekuwa na ukosowaji mkali juu ya namna wasichana hao walioachiwa huru walivyobakia katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, badala ya kujiunga na familia zao. Alhassan amesema wasichana hao wako mjini Auja kwa idhini yao wenyewe.