1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasiwasi mpya watanda Somalia

Thelma Mwadzaya16 Desemba 2010

Hali inaripotiwa kuwa ya wasiwasi nchini Somalia baada ya kitisho kipya cha wapiganaji wa Al Shabaab kuwashambulia wapiganaji wa Hezb al-Islam wa mji wa Afgoyw ulio na wakaazi wengi walioyakimbia mapigano.

https://p.dw.com/p/Qd0L
Wapiganaji wa Al ShababPicha: AP

Kulingana na wakazi wa eneo hilo waliozungumza na shirika la habari la AFP, hali hiyo ya wasiwasi imesababishwa na uhasama kati ya makundi hayo mawili vile vile wapiganaji zaidi walioongezeka mjini Afgoye.

Somalia Stadt Mogadishu
Mji wa MogadishuPicha: AP

Kundi la Al Shabab lililo na mafungamano na lile la Al Qaeda limeyateka maeneo mengi ya eneo la kusini na katikati mwa Somalia na mji wa Mogadishu. Wapiganaji wa Hezb al-Islam walio na misingi ya kisiasa zinazoongozwa na Hassan Dahir Aweys, linayamiliki maeneo ya kaskazini magharibi nje ya mji wa Mogadishu vilevile maeneo ya mbali ya kusini mwa nchi.