1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasiwasi nchini Ivory Coast

Saumu Ramadhani Yusuf1 Desemba 2010

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton, amewataka maafisa nchini Ivory Coast kuyatangaza matokeo ya uchaguzi haraka iwezekanavyo.

https://p.dw.com/p/QNK9
Waziri mkuu wa zamani Alassane Ouattara na wafuasi wakePicha: Picture alliance/dpa

 Rais Laurent Gbagbo tayari ameshapeleka wanajeshi  katika mji mkuu wa nchi hiyo Abidjan. Ufaransa pia imeitolea mwito tume ya uchaguzi kuyatangaza matokeo hayo kabla ya kesho. Rais huyo anashutumiwa na wafuasi wa mpinzani wake, Alassane Quattara, kwa kuyazuia matokeo ya uchaguzi huo wa duru ya pili kutokana na hofu kwamba ameshindwa.

Msemaji kutoka kambi ya upinzani amesema kwamba hatua ya kuyachelewesha matokeo ni jaribio la rais Gbagbo la kutaka kuiba kura na kuingia kwa nguvu madarakani.Tarehe ya mwisho ya kutangaza matokeo hayo kisheria inamalizika saa sita ya usiku wa leo. Zoezi la uchaguzi huo lilitawaliwa na ghasia zilizosababisha mauaji ya kiasi cha watu 12.