1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasiwasi wakumba Kivu Kaskazini uchaguzi unapokaribia

Benjamin Kasemba20 Desemba 2018

Wasiwasi unazidi kuwazonga wakaazi wa mkoa wa Kivu ya kaskazini kuhusiana na machafuko yanayotokea kuelekea uchaguzi.

https://p.dw.com/p/3AQ6y
Demokratische Republik Kongo Wahlkampagne des Kandidaten Félix Antoine Tshilombo Tshisekedi
Picha: Lydie Omanga

Wasiwasi unazidi kuwazonga wakaazi wa mkoa wa Kivu ya kaskazini kuhusiana na machafuko yanayotokea kuelekea uchaguzi.

Ikiwa kumesalia hivi sasa siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu kuendeshwa hapa nchini wengi wa raia waonekana kuwa na wasiwasi huku wakitilia mashaka ikiwa uchaguzi huo utaendeshwa katika hali tulivu kufuatia vurugu zinazo endelea kuripotiwa katika vijiji hususan hapa mkoani kivu ya kaskazini eneo ambalo kwa miongo kadhaa raia wake wanashuhudia vita vya mara kwa mara vinavyo sababishwa na makundi ya wapiganaji wenye kumiliki silaha.

Baadhi wanasema wanahofu na wengine na wengine wanaitaka serikali kuimarisha hali ya usalama wakati wa uchaguzi huu utakaoendeshwa jumapili wiki hii.

Watetezi wa haki za binadamu wanataka serikali kuyazima makundi ya wapiganaji wenye kumiliki silaha.
Watetezi wa haki za binadamu wanataka serikali kuyazima makundi ya wapiganaji wenye kumiliki silaha.Picha: DW/J. Kanyunyu

Upande wao watetezi wa haki za binadamu wameghadhabishwa kuona jinsi gani bado serikali haijafanikiwa kuvitokomeza vikundi vya waasi wa Maimai vinavyo sababisha raia wengi kuyahama makaazi yao na kupata hifadhi ndani ya maeneo yanayokuwa tulivu.

Haya yanajiri wakati ambapo huduma ya kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu yaani SMS imeonekana kukatizwa kwa muda kote nchini DRC kwa sababu zisizofahamika na kusababisha watumiaji wa huduma hiyo ya simu kuilamu serikali kwa kile wanachokiita kuzuia uhuru wa kujieleza.

Hii ni mara ya tatu nchi ya DRC ikiendesha uchaguzi tangu alipochukuwa madaraka rais wa sasa Joseph Kabila na kuandaa uchaguzi wa kwanza mwaka wa 2006 ambapo aliibuka Mshindi na kuliongoza DRC kwa miaka 17. Kabila alitangaza kutowania mhula mwingine wa urais na kumteuwa bwana Emannuel Shadary kugombea kiti cha rais.

Mwandishi:Benjamin Kasemba

Mhariri:Yusuf Saumu