1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watano wauawa, maandamano yaendelea Misri

Thelma Mwadzaya27 Januari 2011

Maandamano ya kuipinga serikali yameingia siku yake ya pili nchini Misri na kusababisha ghasia katika mji mkuu wa Cairo na Suez,ulio bandarini.

https://p.dw.com/p/105k4
Mamia waandamana Cairo kumshinikiza Hosni Mubarak ajiuzuluPicha: AP

Mpaka sasa idadi ya waliouawa kwenye vurumai hizo imefikia watu watano akiwemo afisa mmoja wa polisi.Maelfu ya waandamanaji wanamtaka Rais Hosni Mubarak ajiuzulu baada ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 30.Kulingana na maafisa wa usalama wa Misri,kiasi ya watu 500 wanazuiliwa kwa sasa.Wakati huohuo,Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Guido Westerwelle,ameuelezea wasiwasi wake hususan kudumisha haki za raia wa Misri.Hali hiyo ya Misri inafanana na ile ya Tunisia kulikotokea maandamano yaliyoisababisha serikali kusambaratika mapema mwezi huu.