1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watetezi wa kiti cha rais wawataka wakongomani wapige kura kwa amani

28 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyK

Kinshasa:

Kambi mbili zinazoüigania kiti cha rais katika duru ya pili ya uchaguzi katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, zimetoa mwito wa pamoja wa kuwepo utulivu na kuahidi kudhamini amani na usalama wakati wa uchaguzi.Thomas Luhaka na Vital Kamerhe-ambao ni wakuu wa vyama vya watetezi wawili wa kiti cha urais mabwana Jean Pierre Bemba na Joseph Kabila wametia saini kwa pamoja hati mbili chini ya usimamizi wa kamisheni huru ya uchaguzi CEI.Katika hati hiyo wawakilishi hao wa mabwana Bemba na Kabila wameahidi mbele ya mwenyekiti wa kamisheni ya CEI,Askofu Apollinaire Malu Malu, kuhakikisha uchaguzi unapita katika hali ya amani na utulivu , kuyakubali matokeo ya uchaguzi,kuwahimiza wananchi wavumiliane na kuheshimu utaratibu wa kutangaza matokeo ya uchaguzi.Kampeni ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais imemalizika jana usiku na hali inasemekana ni shuwari wananchi wakijiandaa kuteremka vituoni kesho,kuhitimisha utaratibu mrefu uliolengwa kuleta amani na demokrasia katika nchi hiyo iliyoteketezwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.