1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 11 wamekufa katika ajali ya mto Nile

22 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CfEX

Watu 11 wamekufa maji baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kuanguka kutoka kwenye feri iliyokuwa ikisafiri kwenye mto Nile.

Maafisa wa usalama nchini Misri wanasema maiti 11 zimepatikana baada ya ajali hiyo kutokea karibu na mji wa Minya.

Hii ni ajali ya tatu mbaya kutokea nchini Misri tangu kuanza kwa likizo ya sikukuu ya Idd al Adha Jumanne iliyopita. Wamisri takriban wanane waliuwawa wakati basi walilokuwa wakisafiria lilipogongana na gari lengine hapo jana. Watu wasiopungua 34 walijeruhiwa juzi Alhamisi wakati treni ya abiria ilipoacha reli kwenye kituo kimoja katika kitongoji cha mji mkuu Cairo.

Ajali nyingi nchini Misri hutokea kwa sababu ya madereva kutokuwa waangalifu, sheria za barabarani kutotekelzwa na hali mbaya ya barabara.