1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 14 akiwemo askari wa Marekani wauawa Iraq

21 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CeOg

DIYALA.Mshambuliaji wa kujitoa mhanga amewaua watu 14 akiwemo askari mmoja wa jeshi la Marekani, baada ya kujilipua katika kituo cha kujiandikisha kazi, kwenye mji wa Kanaan nchini Iraq.

Mji huo uko katika jimbo la Diyala ambalo linakabiliwa na ghasia na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo wa al Qaida.

Katika tukio lingine bomu lililotegwa kwenye gari lililipuka karibu na duka la pombe ambapo watatu waliuawa.Duka hilo lilikuwa ni moja kati ya machache yaliyofunguliwa hapo jana katika siku ya maadhimisho ya sikukuu ya Ei del Hadji.

Mjini Washington bunge la Congress limeidhinisha kiasi cha dola bilioni 70 zikiwa ni fedha za ziada kwa ajili ya harakati za kijeshi za Marekani nchini Iraq na Afghanistan.

Kiwango hicho ni chini ya nusu ya kile kilichoombwa na Rais Bush kwa ajili hiyo.Wabunge wengi wa chama cha Democrat bila ya mafanikio walijaribu kuzuia ombi hilo la Rais Bush wakimchagiza kuweka ratiba ya kuyaondoa majeshi ya Marekani nchini Irak.