1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 14 wa familia moja watekwa nyara nchini Iraq

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfry

BAGHDAD:

Watu waliokuwa na bunduki wamewakamata watu 14 wa famila moja nje ya mji wa Baghdad.

Tukio hilo, ambalo limefanywa na watu waliojifanya wanausalama, limetokeoa jumatatu katika eneo la Dilaya linalopatikana umbali wa kilomita 90, kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Baghdad.

Polisi inasema kuwa watu hao wamesimamisha basi dogo lililokuwa limewabeba watu hao katika kizuizi bandia.

Miongoni mwa waliokamatwa ni wanawake pamoja na watoto.Ghasia zimekuwa zimepungua nchini Iraq miezi michache iliopita,lakini maofisa wa Iraq na Marekani, wanaonya kuwa wapiganaji wa kiSunni wa Al –Qaeda wamejikusanya katika maeneo ya Diyala baada ya kufurushwa kutoka Baghdad na vikosi vya Iraq na Marekani.

Kwa mda huohuo watu wasiopungua wawili wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea karibu na ubalozi wa Iran mjini Baghdad.

Idadi ya waliojeruhiwa katika mlipuko huo inatarajiwa kupanda.