1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 14 wauwawa Somalia

21 Februari 2014

Kiasi ya watu 14 wanasemekana kuwawa baada ya kutokea shambulizi la kujitoa mhanga katika makazi ya rais mjini Mogadishu, Somalia.

https://p.dw.com/p/1BDWL
Somalia Anschlag Präsidentenpalast 21.02.2014
Shambulio katika makazi ya rais wa SomaliaPicha: picture alliance/AP Photo

Moja ya vyanzo kutoka polisi nchi humo vinasema waliouwawa katika shambulio hilo la kujitoa mhanga ni maafisa watano wa serikali au wanajeshi pamoja na wapiganaji tisa. Shirika la habari la Ufaransa AFP limemnukuu, afisa mmoja wa polisi nchini Somalia Abdirahman Mohammed akisema wamezihesabu maiti za wapiganaji tisa na maafisa wengine wa watano wakisomali wakiwemo wanajeshi.

Taarifa nyingine kutoka shirika la habari la Uingereza-Reuters kwa kunukuu vyanzo vingine vya polisi zinasema bomu lililokuwa katika gari lilipuka na baadae kufanya walinzi wa amani waingie katika mapigano makali ya kufyatua risasi na wanagmabo wavamizi. Rais wa taifa hilo, Hassan Sheikh Mahamud hajajeruhiwa katika shambilio lililotokea katika eneo lenye ulinzi mkali linalojulikana kama "Villa Somalia"

Taarifa ya mwakilishi wa Umoja wa Mataifa

Hassan Sheikh Mohamud Präsident Somalia
Rais wa Somalia,Hassan Sheikh MohamudPicha: Getty Images

Katika mtandao wake wa Twitter, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa Nick Kay aliandika kwamba rais alimwita na kumweleza kwamba hajajeruhiwa katika shambulio hilo ingawa anasikitika kuwa baadhi kupoteza maisha.

Kumekuwa na taarifa za kutatanisha kuhusu ripoti zinazoelezea mkasa huo. Abdikadir Ahmed, afisa wa polisi mwandamizi aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba mapigano yalitokea katika nyumba ya kamanda wa juu wa jeshi la Somalia, Jenerali Dahiri Aden Indha Qarshe, ambayo ipo katika mazingira ya makazi ya rais na karibu na nyumba ya rais huyo pia.

Mawindo katika nyumba ya ibada

Afisa mwingine wa serikali ambae alikataa kutajwa jinaanasema wanamgamo wapiganaji walifika mpaka katika msikiti uliopo katikati ya eneo hilo la makati ya rais, msikiti ambao kwa kawaida rais anashiriki sala ya Ijumaa. Katibu mkuu katika ofisi ya waziri mkuu wa taifa hilo, ambae pia mkuu wa zamani wa usalama wa taifa ameuwawa sambamba na wapiganaji sita.

Amesema rais hakuwepo msikitini kwa wakati huo ingawa alipanga kwenda. Mtu huyo aliendelea kusema kwa kawaida rais anautumia msikiti huo na ndio maana anahisi walimrenga kiongozi huyo.

Uhakika wa Idadi ya vifo

Idadi ya vifo imeshindwa kuthibitishwa. Vyanzo kutoka katika kitengo cha huduma za dharura vimekana kuingia katika eneo hilo la tukio ambapo majeruhi walipakiwa katika gari la wagonjwa la walinzi wa amani wa Umoja wa Afrika.

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la al Shabab limedai kuhusika na shambulio hilo.

Katika kipindi cha wiki chache zilizopita mji mkuu wa Somalia Mogadishu, kumetokea mfululizo wa mashambulizi ya mabomu ambayo ambayo yanadaiwab kufanya na al Shabaab, kundi ambalo lilifurushwa katika maeneo ya mji huo mwaka 2011 lakini limeendelea na kampeni yao ya vita

Shambulio hilo la Ijumaa linakumbusha kuwa kitisho cha waasi bado kipo na ni namna gani serikali tete ya Somalia bado inapambana kupambana kuweka utawala wa sheria kwa zaidi ya miongoni miwili baada ya kuanguka utawala wa Mohamde Siad Barre,na Somalia kuingia katika vurugu na mapigano.

Mataifa ya Magharibi ambayo yamejitumbukiza kusaidia kumaliza mgogoro wa Somalia yana wasiwasi kwamba huenda, taifa hilo likarejea katika machafuko.

Mwandishi: Sudi Mnette RTR

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman