1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 22 wauwawa Syria

Admin.WagnerD26 Januari 2016

Takribani watu 22 wameuwawa na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa baada ya kutokea miripuko miwili ya mambomu katika mji unaodhibitiwa na serikali wa Homs

https://p.dw.com/p/1HjxC
Syrien Islamistische Kämpfer der Al-Nusra Front
Wapiganaji wa kundi la Al-NusraPicha: Getty Images/AFP/O.H. Kadour

Gavana wa jimbo la Homs Talal Barazi alisema shambulizi la awali lilikuwa la bomu lililotegwa katika gari na kulenga eneo la kituo cha ukaguzi. Baadae kwa mujibu wa chombo cha habari mhanga aliejifunga mkanda wenye viripuzi alijiripua. Jiji la Homs lilikuwa kiini cha vuguvugu la 2011 la kupinga serikali yanayosababisha machafuko nchini Syria

Kudhibitiwa kwa mji wa Sheikh Maskin

Na katika habari ya faraja kwa upande wa majeshi ya serikali yenye kuungwa mkono na mashambulizi ya anga jeshi la Urusi, yamefanikiwa kuurejesha katika himaya yake mji muhimu uliyopo kusini mwa Syria, taarifa ambayo imetangazwa vilevile na makundi ya wanaharakati wa haki za binaadamu nchini humo.

Syrien Madaja Ankunft Hilfskonvoi
Wimbi la wakimbizi wa Syria katika eneo la MadajaPicha: Getty Images/AFP/Stringer

Kudhibitiwa kwa Sheikh Maskin, ambao upo kati ya jiji la Damascus na jimbo la kusini la Daraa, kunatokea siku chache baada hatua kubwa ya kusonga mbele kwa majeshi ya serikali katika kaskazini-magharibi na kabla ya mazungumzo ya amani ambayo yamepangwa kufanyika mjini Geneva, yaliyopangwa kufanyika Ijumaa.

Kwa mujibu wa shirika la uangalizi wa haki za binaadamu nchini Syria, wanajeshi wa Syria na wanamgambo wa Kilebanon wa Hezbollah waliweza kuweka chini ya himaya yao mji wa Sheikh Maskin baada ya mapigano makali.

Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema taifa lake halijamtaka rais Bashar al Assad ajuzulu na wala kutoa fursa ya hifadhi kwa kiongozi huyo baada ya hatua hiyo. Aidha Sergei amgusua suala la maandalizi ya mazungumzo ya amani ya Syria kwa kusisitiza kuwa mazungumzo hayo ya yenye kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa yaliopangwa kuanza wiki hii hayataweza kufanikiwa endapo wawakilishi wa jamii ya Wakurid hawatoalikwa.

Waziri huyo amenukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP akisema pasipo ushiriki la ujumbe wa kundi hilo la watu hakutakuwa na uwezekano wa kupatikana suluhisho madhubuti la kisiasa nchini Syria- Na kuongeza kwamba jambo hilo lipo katika mamlaka ya mjumbe wa umoja wa matiafa katika mazungumzo hayo Staffan de Mistura,ni kundi la upinzani linalopaswa kualikwa.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP/RTR
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman