1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 30 wauwawa katika mazishi.

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CizX

Baghdad.

Kiasi watu 30 wameuwawa na wengine kadha wamejeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga katika mazishi mjini Baghdad. Watu walioshuhudia wamesema kuwa mshambuliaji huyo alilipua milipuko hiyo aliyokuwa ameivaa katikati ya kundi la watu waliokuwa wakiomboleza katika eneo la Washia. Duru zinasema kuwa hilo ni shambulio baya kabisa la bomu kutokea mjini Baghdad tangu Septemba na moja kati ya baya kabisa nchini Iraq kwa muda wa miezi kadha.