1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kadhaa huenda wakachukuliwa hatua Ujerumani kwa ufuska na watoto

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CfrO

BERLIN:

Polisi ya Ujerumani inasema watu wanaofikia elf 12 wanaweza wakachukuliwa hatua za kisheria kwa kuhusika na masuala ya ufuska wa picha na maandhishi ya ngono na watoto.

Polisi inasema kuwa watu wapatao elf moja na mia saba nchini Ujerumani ,wamesha- shtakiwa kwa kupatikana wakiwa na vitu visivyokubaliwa kutokana na msako wao wa mda mrefu.Imeahidi kufanya msako mwingine.

Wakati wa Operesheni hiyo iliopewa jina la Ahera,polisi ilivunja mtandao ambao unasambaza picha za ngono baada ya kudokezewa na mwenye kampuni inyotoa huduma za ya Internet akisema aligundua mtiririko usio wa kawaida wa data na ndio akaiarifu polisi.