1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wawili watekwa nyara Puntland

26 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CgPe

MOGADISHU

Polisi wamepambana kwa kufyatuliana risasi na kundi la wanamgambo waliowateka nyara wafanyikazi wawili wa shirika la madaktari wasio na mipaka katika jimbo lililojitenga la Puntland nchini Somalia.Mapamabano hayo yametokea hii leo katika mji wa Bossasso kaskazini mashariki ya jimbo hilo la Puntland.

Polisi wameanzisha opresheni ya kuwakomboa mateka hao Daktari,raia wa Spain na muuguzi wake kutoka Argentina.Wawili hao walitekwa nyara mapema hii leo wakiwa ndani ya gari na hatma yao haijajulikana.

Jumatatu iliyopita mwandishi habari Gwen Le Gouil aliachiwa huru na watekaji nyara waliokuwa wamemzuilia kwa muda wa wiki moja katika eneo hilo la Puntland.