1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wazanzibari wa Scandinavia waamua kuisaidia nchi yao

26 Aprili 2011

Wazanzibari wanaoishi ng'ambo wafanya mkutano jinsi ya kuchangia katika maendeleo ya nchi yao.

https://p.dw.com/p/113wk
Kisiwa cha ZanzibarPicha: picture alliance/dpa

Wakati leo Watanzania wanaadhimisha mwaka wa 47 tangu kuundwa muungano kati ya Tanganyika na Visiwa vya Zanzibar, mwishoni mwa wiki iliopita huko Copenhagen, Denmark, kulifanyika mkutano wa Wazanzibari katika Diaspora, yaani wanaoishi ng'ambo, upande wa nchi za Scandinavia, kuzungumzia namna wanavoweza kuchangia katika maendeleo ya nchi yao. Hali hiyo inafanyika baada ya kuundwa serikali ya Umoja wa taifa huko Visiwani, na hamu ya wakuu wa serikali hiyo kutumia uzoefu na ujuzi wa Wazanzibari walio ng'ambo katika kulisukuma gurudumu la maendeleo Visiwani. Othman Miraji alizungumza kwa njia ya simu na msemaji wa mkusanyiko huo wa Wazanzibari katika Scandinavia, Dr. Yusuf Saleh...