1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Kouchner wa Ufaransa kukutana na viongozi wa Libanon

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CX4Q

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa,Bernard Kouchner hii leo amerejea Libanon kujadiliana na viongozi wanaohasimiana kuhusu wadhifa wa rais. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Libanon Fouad Siniora imesema,Kouchner atakutana na Siniora.Wakati huo huo kituo cha televisheni cha Libanon kimesema, Kouchner atakutana na viongozi wa serikali inayodhibitiwa na wanasiasa wanaoungwa mkono na mataifa ya Magharibi na pia wapinzani wanaoungwa mkono na Hezbollah.