1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu Cameron apambana na maswali ya wabunge

20 Julai 2011

Waziri mkuu David Cameron ,ametetea uadilifu wake katika mjadala wa dharura bungeni leo,akisema kuwa anasikitika kutokana na mzozo uliosababishwa na kumuajiri mhariri wa zamani wa gazeti ambaye anakabiliwa na kashfa.

https://p.dw.com/p/120RI
Waziri mkuu David Cameron akijibu maswali ya wabunge bungeniPicha: picture alliance/dpa

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron , ametetea uadilifu wake katika mjadala wa dharura bungeni leo, akisema kuwa anasikitika kutokana na mzozo uliosababishwa na kumuajiri mhariri wa zamani wa gazeti ambaye yuko anahusika na kashfa ya kunasa mawasiliano ya simu. Ametangaza wajumbe wa jopo litakaloongozwa na jaji watakaochunguza kashfa hiyo na kusema kuwa kiwango cha kashfa hiyo kimekuzwa kulingana na mzozo huo unaozidi kusambaa.

Akiwekewa mbinyo na wabunge kutaka aombe radhi , David Cameron amesema kuwa , Andy Coulson , msemaji wake wa zamani ambaye aliwahi kuwa mhariri wa gazeti la Rupert Murdoch la News of the World , amekana kufahamu unasaji huo wa mawasiliano ya simu wa gazeti hilo. Lakini iwapo Coulson atakutikana kuwa amedanganya , waziri mkuu amesema hapo ndio ataomba msahama.

Nimekwisha sema wazi kuwa iwapo Andy Coulson alikuwa anafahamu unasaji huo wa mawasiliano katika gazeti la News of the world sio tu kwamba amenidanganya lakini atakuwa ameidanganya polisi, kamati maalum , tume ya malalamiko ya vyombo vya habari na pia kujisafisha binafsi katika mahakama.

News of the World Andy Coulson
Mhariri wa zamani wa News of the World Andy Coulson, ambaye aliajiriwa na waziri mkuu Cameron kuwa mwandishi wa waziri mkuu.Picha: dapd

Iwapo hayo yote yatathibitishwa anaweza kutarajia kupambana na madai mabaya sana ya uhalifu.

Akiwa anashambuliwa kutoka pande zote lakini haonekani kuwa katika kitisho kikubwa cha kuvuliwa madaraka na chama chake baada ya miezi 15 ya kuwapo madarakani , Cameron alitetea uamuzi wake na wa wafanyakazi wanaomzunguka katika kufanyakazi na jeshi la polisi pamoja na himaya ya vyombo vya habari ya Murdoch ya News Corp.

Lakini kiongozi huyo wa chama cha Consevative mwenye umri wa miaka 44 amesema baada ya wiki hizi mbili ngumu katika uongozi wake kuwa, mtu hafanyi maamuzi bina kufikiria, unachukua uamuzi kwa ajili ya baadaye. Unaishi na unajifunza na amini nawaambia nimejifunza.

Cameron ambaye alikatiza ziara yake ya bara la Afrika wakati bunge lilichelewesha mapumziko ya majira ya joto kumuuliza maswali muhimu juu ya kashfa hiyo.

Kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband ambaye uongozi wake ambao umefikisha nusu mwaka hadi sasa kama kiongozi wa upinzani umekuwa kimya mno , umeimarika kutokana na mashambulio yake dhidi ya Cameron kuhusiana na kashfa hii na kusema kumuajiri Coulson ni maafa makubwa ya ukiuamuzi.

Kwanini haendi umbali zaidi badala ya kuomba radhi nusu nusu na kuomba radhi kamili kwa kumuajiri Coulson na kumleta ndani ya ofisi ya Downing Street? Miliband aliuliza. Cameron akajibu.

Watu watatoa hukumu juu ya hili. Ni dhahiri kuwa nimehuzunishwa sana na nasikitika mno juu ya vurumai iliyosababishwa na hali hii.

David Cameron ameteua jopo la wajumbe litakaloongozwa na jaji Brian Leveson litakaloanza kusikiliza kesi hiyo katika muda wa wiki chache zijazo na litawasilisha ripoti yake katika muda wa miezi 12.

Großbritannien Labour Vorsitzender Ed Miliband
Kiongozi wa upinzani bungeni Ed Miliband wa chama cha Labour.Picha: picture alliance / dpa

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / rtre

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman.