1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu Ethiopea ailaumu UN

20 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Ce95

NAIROBI.Waziri Mkuu wa Ethiopea Meles Zenawi ameyalaumu mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuzidisha chumvi habari za kuwepo kwa hali mbaya ya usalama na maisha nchini Somalia.

Akizungumza katika mahojiano na shirika la utangazaji la Uingereza BBC Waziri Mkuu huyo wa Ethiopea amesema kuwa mashirika ya Umoja wa mataifa kwa sasa yamekuwa yakitoa habari zenye kupotosha kuhusiana na hali halisi.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa mapigano kati ya majeshi ya Ethiopea yanayoisadia serikali ya mpito na wanamgambo wa kiislam katika mji mkuu Mogadishu, yamepelekea kuwepo kwa janga kubwa la kibinaadamu nchini humo.Zaidi ya watu laki sita hawana makazi.

Meles Zenawi ambaye majeshi yake mwanzoni mwa mwaka huu yalisaidia kuwafurusha wapiganaji wa kiislam mjini Mogadishu amekanusha ya kwamba majeshi hayo kwa makusudi yamekuwa yakishambulia raia.