1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu Samak Sundarajev atangaza hali ya hatari Bangkok

Saumu Mwasimba2 Septemba 2008

Mtu mmoja ameuwawa katika mapambano makali kati ya wapinzani na wafuasi wa serikali

https://p.dw.com/p/F90t
Waandamanaji wanaoipinga serikali wanamtaka waziri mkuu ajiuzuluPicha: AP

Waziri mkuu wa Thailand Samak Sundararajev ametangaza hali ya hatari katika mji wa Bangkok.

Maafisa wamesema mikutano ya watu zaidi ya watano pia imepigwa marufuku.Akizungumza kupitia redio na televisheni ya taifa waziri mkuu ameliamrisha jeshi kuchukua madaraka ya kuweka amani baada ya kutokea mapambano makali kati ya waandamanaji wanaoiunga mkono serikali na wapinzani wa serikali.

Wanajeshi kiasi cha 400 wamepelekwa katika majengo ya serikali kuzuia mapambano zaidi.Vyombo vya habari pia vimezuiwa kuripoti kuhusiana na mgogoro huo kutokana na kile serikali inachosema vyombo hivyo vinahujumu usalama wa nchi.

Katika mapambano yaliyoibuka jana jioni mtu mmoja aliuwawa na wengine 20 wakajeruhiwa.Wapinzani wa serikali wa chama cha Peoples Alliance For Demokrasi PAD wanaolikalia jengo la serikali wameapa kutoondoka.

Maelfu ya wafuasi wa chama hicho ambao wamekuwa wakiandamana kwa wiki moja sasa wanamtaka waziri mkuu Samak Sundarejev wanayemshutumu kwa kuhusika na ufisadi ajiuzulu kutoka madarakani.