1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa elimu Iran ajiuzulu

2 Desemba 2007

Waziri wa elimu Iran ajiuzulu

https://p.dw.com/p/CVjv

Teheran:

Waziri wa elimu wa Iran amejiuzulu, na kusababisha mabadiliko ya tano ya baraza la mawaziri tangu 2005. Redio ya taifa ilitangaza kujiuzulu huko kwa Bw Mahmoud Farshidi lakini bila ya kutoa sababu ya kujiuzulu kwake. Hata hivyo miaka ya karibuni imeshuhudia maandamano ya waalimu wakidai nyongeza ya mishahara huku maandamano ya mwisho yakitokea mwezi Machi mwaka huu.

Wizara hiyo inayoshughulikia elimu ya juu hadi chuo kikuu, ndiyo kubwa kabisa nchini Iran ikiwa na watumishi kiasi ya milioni moja. Tangu 2005, Rais Mahmoud Ahmedinejad amefanya mabadiliko mara nne katika baraza lake la mawaziri. Mwezi Novemba aliwateuwa mawaziri wapya katika wizara muhimu ya mafuta na viwanda.