1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Afghanistan amepokonywa wadhifa wake

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2m

Kabul:

Bunge la Afghanistan limempokonya wadhifa wake waziri wa mambo ya nchi za nje Rangin Dadfar Spanta.Katika kura ya imani bungeni,wabunge wengi wamesema hawana imani na waziri huyo wa mambo ya nchi za nje.Hoja zinazotolewa ni kwamba Spanta hakufanya chochote kuzuwia kutimuliwa wakimbizi wa Afghanistan toka nchi jirani ya Iran.Pekee mwezi uliopita Iran imewafukuza wakimbizi 50 elfu wa Afghanistan wanaosemekana kuingia nchini humo kinyume na sheria.Afghanistan iliiomba Iran isiwafukuze wakimbizi hao kwa sasa ,kwasababu Kabul haina uwezo bado wa kuwashughulikia.Iran haijaitika mwito huo.Alkhamisi iliyopita,waziri wa Afghanistan anaeshughulikia masuala ya wakimbizi Akbar Akbar alilazimika kujiuzulu baada ya wabuznge kupiga kura ya kutokua na imani nae.Iran inapanga kuwafukuza wakimbizi milioni moja wa Afghanistan.