1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ziarani Mashariki ya kati

14 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fp

Jerusalem / Ramallah:

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice amewasili Jerusalem hii leo katika juhudi za kuandaa mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya Mashariki ya kati.Leo jioni bibi Condoleezza Rice atakutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert.Leo usiku waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Marekani atazungumza na waziri mkuu wa Palastina Salam Fayyad mjini Jerusalem kabla ya kukutana baadae na kiongozi wa utawala wa ndani Mahmoud Abbas.Wakati huo huo juhudi za kidiplomasia kati ya Israel na Palastina zimeshika kasi.Wawakilishi wa tume za Palastina na Israel wanapanga kukutana mara tatu,bila ya kutaja mazungumzo ya papo kwa papo kati wakuu wa tume zao ambao ni Ahmad Qorei aliyewahi kua waziri mkuu wa Palasatina na mkurugenzi wa ofisi ya waziri mkuu wa Israel Yoram TURBOWITZ.Jana mkuu wa tume ya Palastina mazungumzo Ahmad Qorei alizungumza na mjumbe wa Marekani David Welsh na kumuelezea umuhimu wa kutangazwa waraka timamu mwishoni mwa mazungumzo ya amani yatakayoitishwa mwezi ujao nchini Marekani.