1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri atakiwa kujiuzulu Tanzania

19 Februari 2018

Watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania wamemtaka waziri wa mambo ya ndani dokta Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi yake mara moja ikiwa ni sehemu ya kuwajibika kutokana na ukiukwaji wa haki za kiraia nchini humo.

https://p.dw.com/p/2sv6y
Wahlen in Tansania
Picha: DW/E. Boniphace

Mojawapo ya matukio ambayo yameashiria ukiukwaji huo wa haki za binadamu unoajitokeza nchini humo ni jeshi la polisi kutumia risasi za moto kuwatawanya wafuasi wa chadema walioandamana kuelekea ofisi ya mkurugenzi wa uchaguzi kinondoni.

Hayo wameyaweka wazi walipozungumza na dw na kuongeza kuwa, mkurugenzi wa uchaguzi pamoja na mkuu wa jeshi la polisi wanatakiwa kujitathmini katika matukio yaliojitokeza wakati wa uchaguzi mdogo wa jimbo la kinondoni .

Kuna haja ya mkurugenzi wa uchaguzi kujitathmini

Licha ya watu mbalimbali mashuhuri ndani na nje ya nchi kulaani vikali, tukio la kuuwawa kwa risasi msichana wa chuo cha usafirishaji, wakati polisi walipo watawanya waandamanaji waliokuwa na viongozi wa chama cha upinzani chadema wakielekea ofisi za mkurugenzi wa uchaguzi kinondoni kudai barua za mawakala zitakazo watambua wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la kinondoni.

Trauer um Akwilina Akwilini
Marafiki wa msichana aliyepigwa risasi Akwilina Akwilini (kwenye picha) wakimliwaza dadakePicha: DW/E. Boniphace

Watetezi hao wa haki za binadamu wameiambia DW kuwa kuna haja ya waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani, mkurugenzi wa uchaguzi pamoja na mkuu wa jeshi la polisi kujitathmini na kuwajibika kwa wananchi kutokana na matukio ya utekaji,uteswaji pamoja na mauaji kutokea.

Onesmo ole ngurumo mratibu wa kitaifa wa mtandao wa watetezi wa haki a binadamu Tanzania, anasema kuwa, mbali na kumtaka waziri nchemba kujiuzulu lazima tume huru iundwe kuchunguzwa kwa kifo cha binti Akwilina Akwilina aliepigwa risasi wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji walioongozana na viongozi wa chadema kuelekea kwa mkurugenzi wa uchaguzi juma lililopita.

Mkuu wa kituo cha sheria alishutumu jeshi la polisi

Lakini watetezi hao wanasema kuwa, huenda nchi ya Tanzania hasa katika awamu hii ya uongozi haikubali mfumo wa vyama vingi, hatua ambayo mamlaka zinatumia nguvu nyingi kuuzorotesha mfumo huo ambapo inaleta hofu kwa wananchi hasa nyakati ya chaguzi mbalimbali.

Schwester von  Akwilina Akwilini mit tansanischer Bildungsministerin Joyce Ndalichako
Waziri Joyce Ndalichako akimliwaza dadake marehemu Akwilina AkwiliniPicha: DW/E. Boniphace

Dokta Helen Kijobisimba ni mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu amelishutumu moja kwa moja jeshi la polisi kutokana na kile alichokiita kutaka kujiondoa katika hatia ya mauaji ya binti mdogo wakati wa kuwatawanya waandamanaji

Matamko mbalimbali ya serikali yametolewa kupitia wizara mbalimbali, yakionesha kusikitishwa na kifo cha kwilina Akwilina, huku rais wa amhuri ya muungano wa tanzania kupitia ukurasa wake wa twitter ameziagiza viombo vya dola kufanya uchunguzi wa mapema na hatua stahiki za kisheria zichukuliwe.

Mwandishi: Hawa Bihoga

Mhariri: Yusuf Saumu