1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa nje wa Marekani yuko njiani kwenda Tblissi

Hamidou, Oumilkher14 Agosti 2008

Urusi yalaumiwa kuyaendeya kinyume makubaliano ya kuweka chini silaha huko Georgia

https://p.dw.com/p/ExAk
Jeshi la Urusi nchini GeorgiaPicha: AP




Georgia imeituhumu Urusi kuvunja makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa chini ya upatanishi wa umoja wa Ulaya.Moscow inakanusha tuhuma hizo katika wakati ambapo mashahidi wanazidi kuzungumzia juu ya mapigano katika miji ya Gori na Poti nchini Georgia.


Mnamo siku ya sita ya mzozo wa Caucasus,rais George W. Bush amezungumzia uungaji mkono wake "usiotetereka" kwa serikali ya Georgia akiongeza kusema anamtuma waziri wake wa mambo ya nchi za nje Condoleezza Rice mjini Tblissi.


Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Marekani,atatuwa kwanza nchini Ufaransa,huko Fort de Bregancon kwa mazungumzo pamoja na rais Nicholas Sarkozy.


Kasri la Elysee limesema rais Sarkozy amepokea hakikisho kutoka kwa kiongozi mwenzake wa Urusi Dmitri Medvedev kwamba Moscow itaheshimu ahadi zilizofikiwa kuhusu makubaliano ya kuweka chini silaha.


Hata hivyo rais George w. Bush aliyezungumza kwa simu leo asubuhi  na rais mwenzake wa Georgia ,Mikhail Saakachvili,anazungumzia hofu kutokana na ripoti za kuendelezwa opereshin i za kijeshi za Urusi nchini Georgia.


"Tunasisitiza,milki na umoja wa taifa la Georgia viheshimiwe"-amesema rais Bush na kuongeza tunanukuu:"Urusi lazma iheshimu ahadi ilizotoa na ichukue hatua za kuumaliza mzozo uliopo."Mwisho wa kumnukuu rais George W. Bush wa Marekani.


Matamshi sawa na hayo yametolewa pia na waziri wake wa mambo ya nchi za nje bibi Condoleeza Rice aliyesema:


"Cha muhimu kwa sasa ni kuikumbusha Urusi inawaajibika kuzuwia harakatai zake za kijeshi,kuikumbusha Urusi isiendeleze harakati zinazoweza kutishia umoja wa milki ya Georgia,iachilie mbali matamshi yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa nchi hiyo dhidi ya serikali iliyochaguliwa kwa njia za kidemokrasi nchini Georgia.Wakati umewadia wa kuacha yote hayo."


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Bibi Condoleezza Rice amekwenda umbali wa kutishia  Urusi inaweza kujikuta ikitengwa zaidi pindi ikishindwa kuheshimu makubaliano ya kuweka chini silaha-.


Moscow imekanusha ripoti kwamba vikosi vyake na vifaru vimeingia njiani kuelekea Tblissi au kwamba wanajeshi wake wanapora mali huko Gori,kama alivyodai hapo awali rais Mikhail Saakachvili wa Georgia.


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Serguei Lavrow amemhakikishia waziri mwenzake wa Marekani,hatua kali zitachukuliwa ikidhihirika kwamba kweli visa vya uharibifu vinafanyika.


Kwa upande wa kiutu ndege ya Marekani chapa C-17 ikisheheni misaada ya kiutu imeondoka katika kituo cha kijeshi cha Marekani mjini Ramstein nchini Ujerumani,kuelekea Tblissi.Ndege nyengine iliyosheheni misaada hiyo ya kiutu inatazamiwa kuondoka baadae hii leo.