1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani kuwasilisha barua ya kujiuzulu

Aboubakary Jumaa Liongo9 Februari 2009

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Michael Glos amesema kuwa atawasilisha hii leo kwa Kansela Angela Merkel barua ya kujizulu.

https://p.dw.com/p/GpmI
Michael GlosPicha: AP

Hatua hiyo inafuatia mkutano uliyokuwa na mzozo kati yake na kiongozi wa chama cha  Christian Social Union CSU Horst Seenhofer mjini Munich.  


Waziri huyo wa Uchumi wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 64 aliomba kujipumzisha kutokana na umri wake na kukitaka chama hicho cha CSU kujitizama upya.


Vyombo vya habari vya hapa Ujerumani vimetabiri ya kwamba huenda Waziri wa fedha wa Jimbo la Bavaria Georg Fahrenschon au Katibu Mkuu wa Chama cha CSU Karl Theodor zu Guttenberg.


Kutoelewana huko katika serikali ya shirikisho la Ujerumani kumekuja mnamo wakati ambapo uchumi wake unakabiliwa na mtikisiko mkubwa kuwahi kuikumba toka kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia na pia miezi saba tu kabla ya uchaguzi mkuu.


Ujerumani ndiyo yenye uchumi mkubwa kabisa barani Ulaya

 LINK: http://www.dw-world.de/dw/article/0,,4012222,00.html