1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Uganda akosolewa kuwahusisha wanawake na utalii

Lubega Emmanuel7 Februari 2019

Mpango wa wizara ya utalii Uganda pamoja na kundi moja la wanawake kufanya mashindano ya wanawake walio na maumbo makubwa umekosolewa vikali na makundi ya wanawake na umma kwa jumla.

https://p.dw.com/p/3CvQ2
WM Anschlag Uganda Parlament Flaggen Halbmast Terrorismus
Picha: AP

Mpango wa wizara ya utalii Uganda pamoja na kundi moja la wanawake kufanya mashindano ya wanawake walio na maumbo makubwa umekosolewa vikali na makundi ya wanawake na umma kwa jumla. Wengi wameutaja mpango huo kuwa unaodunisha hadhi ya mwanamke kama chombo cha starehe tu. Hii ni kufuatia tamko la waziri huyo wa Utalii kwamba wanawake wa Uganda wana maumbo ya kipekee yanayoweza kuvutia watalii zaidi kuzuru Uganda.

Kulingana na waziri wa nchi wa utalii Geofrrey Kiwanda wanawake wa jamii zote za Uganda wana maumbile ya kipekee ambayo ni nadra kuonekana sehemu zingine za dunia na ndiyo maana wanaweza kuwa kivutio kikubwa cha utalii.

Lakini matamshi hayo yameibua shtuma kali kutoka kwa wanawake mbalimbali wakimtaja kuwa mtu aliyewavunjia heshima kwa kutaka wao kuwa kivutio cha utalii kutokana na maumbo yao.

Hata hivyo kuna wanawake wanaodai kuwa waziri huyo hajakosea katika kujenga fikra ya kufahamisha dunia kuhusu urembo wa kiafrika ikilinganishwa na mashindano yanayowaonesha wanawake wembamba kuwa ndiyo warembo. Fatuma Omar ambaye ni mwanahabari anasema.

Kwa mujibu wa waziri Geofrrey Kiwanda, wanawake wa jamii za Uganda wana maumbile ya kipekee ambayo ni nadra kuonekana sehemu zingine za dunia na ndiyo maana wanaweza kuwa kivutio kikubwa cha utalii.
Kwa mujibu wa waziri Geofrrey Kiwanda, wanawake wa jamii za Uganda wana maumbile ya kipekee ambayo ni nadra kuonekana sehemu zingine za dunia na ndiyo maana wanaweza kuwa kivutio kikubwa cha utalii.Picha: Imago/photothek

Kufuatia matamshi ya waziri huyo, watu mbalimbali hata kutoka mataifa jirani ya Kenya Tanzania na Rwanda wamesambaza picha za wanawake walioumbika kwenye mitandao ya kijamii kana kwamba mashindano yenyewe yameanza. Si tu wanawake waliojitokeza kumshtumu waziri huyo lakini pia wanaume na wanasiasa wenzake ambao wametisha kuitisha kura ya kumfuta kazi kama waziri.

Hii si mara ya kwanza kwa waziri huyo kuwatumia wanawake katika kunadi Uganda kama kivutio cha utalii. Aliwahi kumhusisha aliyekuwa mke wa msanii Diamond Platinum Zari Hussein kuwa balozi wa kutangaza Uganda chini ya mkakati wake ujulikanao kama ‘Tulambule'Kulingana na mpango wa tamasha hilo linalopangwa kufanyika mwezi ujao, wanawake wanaoamini kuwa wana maumbo ya kuvutia wamealikwa kushindana.

Mwandishi: Lubega Emmanuel DW Kampala.

Mhariri: Iddi Ssessanga