1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wen Jiabao aanza ziara Ujerumani

Saumu Ramadhani Yusuf27 Juni 2011

Ujerumani na China zinatarajiwa kujadiliana kwa kina na serikali ya Ujerumani juu ya masuala ya haki za binadamu na Uchumi hasa kufuatia kubanwa na madeni,Ugiriki.

https://p.dw.com/p/11k8I
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiamkiana na waziri mkuu wa China Wen JiabaoPicha: picture-alliance/dpa
Ziara hiyo ya Wen Jiabao inafanyika ikiwa ni siku nne baada ya kuachiliwa huru kwa mwanaharakati wa upinzani Hu Jia na msanii maarufu nchini humo, Ai Wei Wei. Hatua hiyo ya China imeonekana kama juhudi za kutaka kumalizika mivutano kati ya China na Jumuiya ya Kimataifa juu ya suala la haki za binadamu.

Ziara ya waziri mkuu wa China Wen Jiabao nchini Ujerumani inatazamiwa kugubikwa na suala la haki za binadamu, hasa baada ya kuachiliwa huru mwanaharakati wa upinzani, Hu Jia, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa serikali ya China. Mwanaharakati huyo ambaye amepigwa marufuku kujiingiza katika masuala yoyote yakisiasa, ikiwemo kuzungumza na vyombo vya habari, alitiwa ndani kwa zaidi ya miaka mitatu kwa tuhuma za kuendesha harakati za kutaka kuipindua serikali. Kufuatia ziara hiyo ya Wen Jiabao mjini Berlin, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Guido Westewelle, amefungua rasmi mdahalo juu ya haki za binadamu, akisema kwamba uhusiano wa Ujerumani na China unazingatia masuala mengi, ikiwemo mengine ambayo yameonekana kuzusha tofauti kati ya nchi hizo mbili. Kwa maneno mengine, Westerwelle amesema Ujerumani itazungumza mambo mengi na China, ikiwemo yale ambayo yanaweza suala la uhuru wa kutoa maoni na wa kufanya maandamano pamoja na suala zima la haki za binadamu. China imekuwa ikikosolewa miaka yote na jumuiya ya Kimataifa juu ya suala hilo la haki za binadamu, ingawa katika miezi ya hivi karibuni imeonekana kuregeza kiasi msimamo wake, hasa ikizingatiwa hatua ya kuwaachia huru wakosoaji wake wawili hivi karibuni. Hata hivyo, mashirika ya kupigania  haki za binadamu yanatilia shaka hatua ya china juu ya kuachiliwa huru kwa mwanaharakati wa upinzani Hu Jia.

Wen Jiabao China EU GIpfel Brüssel
Wen JiabaoPicha: AP

Aidha ziara ya Wen Jiabao Ujerumani itaaangazia pia suala la kiuchumi. Tayari serikali ya China leo imetangaza kwamba inamuunga mkono Christian Largard kuchukua nafasi ya mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha la Kimataifa IMF. Hata hivyo, upande mwingine kinachotazamiwa kujadiliwa zaidi kati ya Wen Jiabao na Kansela Angela Merkel hapo kesho, jumanne, ni mtafaruku ulioingia barani Ulaya kutokana na mzigo wa madeni wa baadhi ya nchi za Umoja huo. Hali ya uimara ya sarafu ya Yuro  kwa hivi sasa pia ni kingine ambacho kinaweza kuivutia China na Ujerumani kwa pamoja. Eberhard Sandschneider mtaalamu kutoka jumuiya ya Ujerumani inayohusika na masuala ya kigeni amesema ''Matarajio ya moja kwa moja kwamba China inaweza kusaidia kuiokoa Ugiriki na sarafu ya Euro ni jambo ambalo, kwahakika kabisa, haliwezi kutangazwa wazi. Na hasa kutokana na kwamba hayo yatakuwa sio mazungumzi ya kibishara ya pande mbili, yaani China na Ujerumani, bali yatakuwa ni mazungumzo yanayojumuisha nchi nyingi, mahali ambapo China itakaa na Umoja wa Ulaya italazimika kuwa makini''.

David Cameron Wen Jiabao China
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron,na waziri mkuu wa China Wen JiabaoPicha: AP

Waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, jana alikuwa nchini Uingereza ambako alifikia makubaliano na serikali ya waziri mkuu Cameroon ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya nchi zao mbili,