1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa Umoja wa Ulaya azinduwa mpango mpya wa wakimbizi

9 Septemba 2015

Ameyataka mataifa ya ulaya yakubaliani ifikapo mapema mwiki ijayo jinsi ya kugawana wakimbizi 160,000 walioko katika nchi walikoingilia.

https://p.dw.com/p/1GTXZ
Jean-Claude Juncker EU-Kommissionspräsident 09/2014
Rais wa Umoja wa ulaya Jean-Claude JunkerPicha: Imago

Jean-Claude Junker ambaye alikuwa akizungumza katika bunge la Ulaya mjini Strasbourg, alisema suala sio tena kuwasafirisha lakini wakati umefika wa Umoja huo kuwa na mpango madhubuti na hatua imara. Katika hotuba yake ilioshangiriwa na wabung , Junker akayataka mataifa ya Umoja wa Ulaya yazingatie maadili ya kihistoria wakati yakikabiliana na mmiminiko mkubwa wa wakimbizi tangu vita vya pili vya dunia, wengi wakikimbia vita nchini Syria.

Junker akaongeza kwamba Ulaya inapaswa kuwachukuwa wakimbizi 160,000 mikononi mwake na hilo linapaswa kuwa ni wajibu. Akawataka mawaziri wa ndani wafikie makubaliano kuhusu mpango huo watakapokutana Septemba 14.Mkuu huyo wa Umoja wa ulaya alikuwa akigusia juu ya mpango mpya wa kugawana idadi ya wakimbizi kwa ajili ya makaazi ya dharura kwa wakimbizi 120,000 walioko katika nchi zilizobanwa na tatizo hilo-Italia, Ugiriki na Hungary- sambamba na mpango sawa na huo kwa wakimbizi 40,000 walioko Italia na Ugiriki ambayo ulizuinduliwa mwezi Mei.

Atoa onyo kwa mataifa:

Lakini pamoja na hayo akayaonya mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya dhidi ya kuwabaguwa wakimbizi kwa misingi ya dini zao, pale wanapoamuwa kuwachukuwa na akakumbusha juu ya kuandamwa watu kidini kulikotokea Ulaya miaka iliopita. Akasisitiza, “hakuna dini, hakiuna imani, hauna falsafa panapohusika na wakimbizui. Hatubakuwi.” Na kwa nchi zinazokandamiza haki za kiraia alikuwa na ujumbe huu, "Nimekuwa na yakini kwamba hii ni changamoto itakayoamuwa mustakbali wa ulaya kama tutaendelea kukubaliwa kama bara la maadili na uhuru wa mtu. Hatuwezi tu kusema Syria ni mbali na hatuta lishughulikia tatizo hili."

Merkel auunga mkono mpango huo:

Itakumbukwa mnamo wiki iliopita Waziri mkuu wa Hungary Victor Urban alionya kwamba wimbi la wakimbizi wengi wakiwa ni Waislamu linatishia kuhujumu mizizi ya Ukristo barani ulaya, hoja ambayo ilipingwa vikali na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.Awali akizungumzia mgogoro huo kansela Merkel ambaye ameshauunga mkono mpangob vwa mkuu wa alisema , " Nimekuwa na yakini kwamba hii ni changamoto itakayoamua mustakbali wa ulaya kama tutaendelea kukubaliwa kama bara la maadili na uhuru wa mtu. Hatuwezi tu kusema Syria ni mbali na hatota lisghughulikia tatizo hilo."

Jean-Claude Juncker Waziri mkuu huyo wa zamani wa Luxembourg alitoa wito wa kuchukuliwa juhudi za ziada kubadili sheria za kitaifa ili kuwaruhusu wakimbizi kufanya kazi, tangu siku ya kwanza ya kuwasili kwao, kwa kuzingatia kwamba kazi ni Utu.Alisema mkataba wa Schengen unaoruhusu kutembea katika nchi wanachama bila ya hati ya kusafiria, hautaathirika pamoja na kuwepo kwa hali ngumu inayotokana na mmiminiko wa wakimbizi katika nchi za ukanda huo.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman,afp

Mhariri: Mohammed Khelef