1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Westerwelle awataka Wapalestina wazungumze na Waisraeli

27 Septemba 2011

Westerwelle ameunga mkono mpango wa pande nne zinazoshughulikia mzozo wa Mashariki ya Kati, zikiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi.

https://p.dw.com/p/12guq
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido WesterwellePicha: dapd

Waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Ujeramani, Guido Westerwelle, amewatolea mwito Wapaletina warejee kwenye meza ya mazungumzo na Waisraeli kabla kudai taifa lao. Kwenye hotuba yake aliyoitoa katika Umoja wa Mataifa, waziri Westerwelle amesema Ujerumani inaunga mkono suluhisho la mataifa mawili, na kwamba imedhihirisha msimamo huo kupitia msaada wake kwa serikali ya mamlaka ya ndani ya Wapalestina. Kiongozi huyo aidha amesema taifa la Palestina linaweza tu kupatikana kupitia mazungumzo na viongozi wa Israel.

Rede Mahmoud Abbas UN
Rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud AbbasPicha: dapd

Rais wa mamlaka ya ndani ya Palaestina, Mahmoud Abbas, aliwasilisha rasmi ombi la uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa Ijumaa iliyopita na kuna uwezekano mkubwa ombi hilo likaidhinishwa katika baraza kuu la umoja huo. Hata hivyo Marekani inasema itatumia kura yake ya turufu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupinga ombi hilo kukiwa na haja ya kufanya hivyo.