1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yasitisha huduma zake kwa muda Beni

Amina Mjahid
26 Juni 2019

Shiririka la afya ulimwenguni, WHO lilitangaza tangu jana Jumanne kusitisha kwa muda shughuli zote za kutoa huduma kwa wakaazi katika wilaya ya Beni inayoathiriwa na ugonjwa hatari wa Ebola.

https://p.dw.com/p/3L7gC
Uganda Ebola
Picha: picture-alliance/AP Photo/Al-hadji Kudra Maliro

Tangazo hilo limesababisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa raia wanaoishi katika miji ya Butembo na Goma eneo ambako kampeni za kujilinda na maradhi ya Ebola zimekuwa zikiendeshwa.  

Mkuu wa operesheni za dharura za WHO barani Afrika Yao Michel amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya vijana waendesha bodaboda kuliunguza gari la wahudumu wa kupambana na Ebola Jumatatu wiki hii, ambapo wanne miongoni mwao walijeruhiwa, na gari hilo kuteketea.  

Michel ameiambia DW kuwa huduma za shirika lake zitaanzishwa tena pale hali ya usalama itakapoboreka. Wakazi wa wilaya ya Butembo wameiomba serikali ya Kongo kuingilia katikurejesha huduma dhidi ya Ebola na kuuzuia ugonjwa huo kusambaa zaidi.

Chanzo: Reuters