1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wiki hii michezoni: Mashindano ya Ulaya yafikia robo fainali

Deo Kaji Makomba
10 Agosti 2020

Soka la Ulaya linaingia katika hatua ambayo haijazoeleka wiki hii huku mechi za robo faina za ligi ya mabingwa na ligi ya Ulaya zikichezwa mjini Lisbon na magharibi mwa Ujerumani mtawalia.

https://p.dw.com/p/3gknP
UEFA Champions League Auslosung Manchester City - Real Madrid
Picha: picture-alliance/empics/N. Potts

Mfumo unaofanana na ule wa mashindano ya kombe la dunia la kandanda umelazimika kutumika na bodi inayoongoza shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA, kwa sababu ya janga la virusi vya Corona na umuhimu wa kukamilisha mambo haraka kabla ya misimu ya ligi za ndani kuanza tena mnamo mwezi Septemba.

Hakutakuwa na mashabiki watakaoruhusiwa kutazama mechi viwanjani huku changamoto kwa afya ya umma zikiendelea kutokana na virusi vya Corona. Taarifa ya vipimo vya wafanyakazi wawili wa klabu ya Atletico Madrid ikionyesha kuwa na maambukizi ya corona inaifanya hali kuwa ngumu zaidi.

Robo fainali ya Mabingwa

Katika michezo ya ligi ya mabingwa, robo fainali ya kwanza itakayokuwa na duru moja tu ya mechi badala ya duru mbili kama ilivyozoeleka, itachezwa katika uwanja wa Benfica kati ya Atalanta na Paris Saint-Germain siku ya Jumatano.

UEFA Champions League Plakat Atletico Madrid
BAngo lenye wachezaji soka wa klabu ya Athletico Madrid.Picha: picture-alliance/AP Photo/P. White

Itafuatiwa na mechi kati ya Atletico Madrid na RB Leipzig siku ya Alhamisi katika uwanja wa Sporting Lisbon, ikichukuliwa kwamba Wahispania wataruhusiwa kucheza baada ya wafanyakazi wawili wa timu yao kupimwa na kukutwa na maambukizi ya viruso vya corona.

Soma pia UEFA: Atletico na Leipzig kucheza kama kawaida

Watu hao wawili ambao majina yao hayakutajwa wamewekwa katika karantini na klabu inafanya vipimo kwa wafanyakazi wake wote kwa ajili ya safari ya kuelekea Ureno kwa mara nyingine tena.

Bayern Munich inachuana na Barcelona katika mchezo wa marudiano katika uwanja wa da Luz wa Benfica siku ya Ijumaa.

Mabingwa hao wa Ujerumani wanajiandaa katika kambi yao walioiweka katika eneo la bahari ya Atlantiki kusini mwa Ureno. "Tunayo tu Barcelona kwenye akili zetu," alisema mshambuliaji Robert Lewandowski, mwenye magoli13 hadi sasa na anapania kufikia rekodi ya msimu wa Ligi ya Mabingwa ya mabao 17 iliyowekwa na Cristiano Ronaldo.

Champions League - Juventus v Olympique Lyonnais | Cristiano Ronaldo
Christiano Ronaldo.Picha: Imago Images/LaPresse/Alpozzi

Manchester City inakutana uso kwa uso na Lyon katika mojawapo ya michezo minane ya mwisho siku ya Jumamosi katika uwanja wa Jose Alvalade na mshindi katika mchezo huo atakabiliana na Barca au Bayern katika mechi ya nusu fainali.

Inter Milan uso kwa uso na Bayer Leverkusen

Katika ligi ya Ulaya, Inter Milan wana miadi na Bayer Leverkusen baadaye Jumatatu huko Dusseldorf wakati huko Cologne, uwanja utakaochezwa fainali, washindi wa mwaka 2017 Manchester United wanakipiga na Copenhagen katika mchezo mwingine wa robo fainali.

Soma pia Verstappen aponyoka na ushindi wa Silverstone

Nazo tetesi za uhamisho zinazidi kuenea kuhusu mchezaji wa Leverkusen Kai Havertz wakati Manchester United pia wakiwa wamehusishwa sana na mchezaji wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho. Ripoti za vyombo vya habari zinasema tarehe ya mwisho iliyowekwa na Dortmund ya Agosti 10 imedharauliwa na maafisa wa Old Traord.

Wolverhampton Wanderers inacheza na Sevilla siku ya Jumanne mjini Duisburg wakati Shakhtar Donetsk ikisubiri kukabana koo na Basel huko Gelsenkirchen.

Chanzo: DPA