1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wimbi la machafuko laendelea nchini Kenya

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyPR

NAIVASHA: Si chini ya watu 10 wameuawa hii leo katika mapambano yaliyozuka katika Bonde la Ufa nchini Kenya huku Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan akijaribu kutenzua mgogoro wa mwezi mmoja nchini humo.Ripoti kutoka Naivasha zinasema watu 6 wamechomwa moto na 4 wengine wameuawa kwa kupigwa mapanga.

Sasa si chini ya watu 60 wameuawa katika machafuko ya siku mbili zilizopita magharibi mwa Kenya.Takriban watu 800 wameuawa na kama watu laki mbili na nusu wamekimbia makaazi yao tangu kuzuka kwa machafuko yanayohusika na matokeo ya uchaguzi wa rais.