1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wingu la jivu la volkanu laendelea kuchafua misafara ya ndege

18 Aprili 2010

Misafara ya ndege katika sehemu kubwa ya Ulaya, imepooza kwa siku ya nne mfululizo hii leo. Hii inatokana na wingu la jivu linalopaa hewani kutoka volcano nchini Iceland.

https://p.dw.com/p/MzXV
Passengers queue in a terminal at Germany's largest airport in Frankfurt, central Germany, Friday, April 16, 2010. The airport was closed early Friday due to a cloud of volcanic ash in the upper atmosphere above much of Europe, emanating from a volcanic eruption Eyjafjallajokull glacier in Iceland. The volcanic ash is a hazard to jet aircraft engines, causing the cancellation of many flights over European airspace. (AP Photo/Michael Probst)
Abiria walionasa uwanja wa ndege wa Frankfurt, Ujerumani.Picha: AP

Lakini, safari za ndege za majaribio zilizofanywa nchini Uholanzi na Ujerumani, ikidhihirika bila dhara zozote, zatoa matumaini mema.

Nchi nyingi zimepiga marufuku misafara ya ndege katika anga zao hadi usiku wa manane leo Jumapili au kesho Jumatatu . Hii imewafanya maalfu ya abiria kunasa sehemu mbali mbali ulimwenguni.

Mtaalamu wa utabiri wa hali ya hewa, Helmut Malewski amearifu kwamba wingu hilo la jivu yamkini lisienee mbali zaidi.

Uingereza, imepanua marufuku ya misafara yake mingi ya ndege, hadi saa mbili leo usiku. Anga ya Ujerumani, kwa misafara ya ndege, itafungwa kwa misafara hadi alao alasiri ya leo.

Magari moshi zaidi yanatumika sehemu mbali mbali za Ujerumani, ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wasioweza kusafiri kwa ndege. Maafisa wa mashirika ya ndege wanarifu kwamba, hasara waliopata inapindukia Euro milioni 150 kwa siku.

Mwandishi: Ali,Ramadhan

Mhariri: P.Martin