1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wito kuondosha vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran

14 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbVB

NEW YORK: Iran imetoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kuondosha vikwazo vyote vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo kuhusika na mradi wake wa nyuklia.Katika barua iliyowasilishwa kwa Katibu Mkuu Ban Ki Moon, Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa Mohamed Khazee amesema,mradi wa nyuklia wa Iran ni kwa matumizi ya amani tu.Amesema,ripoti iliyotolewa hivi karibuni na idara za upelelezi za Marekani kuhusu harakati za kinyuklia za Iran imedhihirisha kuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa makusudi lilipotoshwa na kushinikizwa na Marekani,kuchukua hatua za udhalimu dhidi ya Iran.