1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani yashughulikia kutekwa Mjerumani.

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdAp

Berlin.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani imeunda timu ya kushughulikia mzozo itakayoshughulika na kutekwa nyara kwa mfanyakazi wa zamani wa shirika la kutoa misaada la Ujerumani na familia yake nchini Afghanistan. Kwa mujibu wa ripoti za polisi wa Afghanistan , mtu huyo Harald Kleber mwenye umri wa miaka 42 pamoja na mke wake na mtoto walitekwa nyara katika jimbo la magharibi la Herat siku ya Jumapili usiku. Kleber amekuwa akiishi nchini Afghanistan tangu mwaka 2003 ambapo alisilimu na kuwa Muislamu na ameoa mwanamke wa Kiafghanistan. Maafisa wa Afghanistan wamesema kuwa wanaamini kukamatwa huko ni kutokana na mzozo wa kifamilia na kwamba Taliban hawahusiki.