1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wizi wa maandiishi wautia kiwingu mkutano wa Republikan

19 Julai 2016

Donald Trump anakabiliwa na kashfa ya wizi wa maandishi au mawazo iliochafuwa hotuba ya mke wake Melanie katika mkutano mkuu wa chama cha Repuplican ambao ufunguzi wake umekumbwa na vurugu za wanachama wa kawaida.

https://p.dw.com/p/1JRMp
Picha: Reuters/M. Segar

Ulikuwa ni mwanzo mgumu hapo Jumatatu (18.07.2017) kwa mkutano huo wa siku nne kumjengea hoja Trump kwa uteuzi wa kuwania urais wa Marekani kwa tiketi ya chama hicho ambao ulikuwa umesarifiwa ili vyombo vya habari vimnadi kwa mapana mgombea huyo na wafuasi wake.

Wakati mamilioni ya watu wakiuangalia mkutano huo majumbani mwao kupitia televisheni Melania Trump ametowa hotuba ya kumtetea mume wake na juhudi zake za kuwa rais mpya wa Marekani mbele ya kadamnasi ya maelfu ya wajumbe wa chama wa Repuplikan waliohudhuria mkutano huo mkuu ulifanyika Cleveland hapo jana usiku.

Mke wa Trump ambaye ni mzaliwa wa Slovenia hadi sasa alikuwa hajitokezi sana katika kampeni lakini hapo jana alipanda jukwaani akiwa kama mpiga debe mkuu wa mume wake na alipanda jukwaani na taswira kamili ya mrembo wa zamani wa mitindo.

Trump ndiye anayewafaa

Amesema Donald ni na daima amekuwa kiongozi mzuri na sasa atafanya kazi pamoja na wananchi.Amesema mume wake huyo sio mtu wa kukata tamaa na amemueleza kama ni baba mwenye mapenzi na mfanya baishara mwenye mafanikio ambaye atakuwa rais imara na mwenye stahmala.

Mkutano mkuu wa chama cha Repuplikan Clevaland..
Mkutano mkuu wa chama cha Repuplikan Clevaland..Picha: Reuters/C. Allegri

Amewahakikishia wajumbe kwamba iwapo wanataka kuwa na mtu ambaye atawapigania pamoja na kuipigania nchi yao basi Trump ndiye anayewafaa.

Lakini kile kilichobainika ni kuwepo kwa matamshi yanayofanana kabisa katika sehemu ya hotuba yake hiyo kuhusu maadili yanayomungoza sawa na aliyoyatowa Michele Obama katika mkutano mkuu wa chama cha Demokratik kumteuwa mume wake kuwania urais wa Marekani hapo mwaka 2008.

Wizi wa maandishi

Melanie amesema "Tokea ujanani wazazi wangu walinivutia kwa maadili ya kufanya kazi kwa bidii kwa kile unachokitaka katika maisha.Kwamba neno lako ni dhamana yako na unatenda kile unachosema na kutimiza ahadi zako. Kwamba unawaheshimu watu na kuonyesha desturi na maadili katika maisha ya kila siku.Haya ni mafunzo ambayo tunaendelea kuyarithisha kwa mtoto wetu wa kiume leo hii na tunatakiwa kuyarithisha kwa vizazi vingi vijavo"

Michelle Obama( kulia) na Melania Trump
Michelle Obama( kulia) na Melania TrumpPicha: picture-alliance/dpa

Mara tu baada ya kuitowa hotuba hiyo ilikuja kuwekewa kiwingu baada ya kubainika kwamba matamshi hayo ulikuwa ni wizi wa maandishi au mawazo kwani yalikuwa ni matamshi yaliyotolewa na Michelle Obama wakati wa uteuzi wa mume wake hapo mwaka 2008.

Jason Miller mshauri mwandamizi wa masuala ya mawasiliano wa Trump alikiri katika taarifa kwamba timu ya waandishi ya Melania Trump mara nyengine walikuwa wakiingiza mawazo yake mwenyewe binafsi katika hotuba zake.

Mkutano huo ulianza kwa vurugu baada ya wajumbe wanaompinga Trump kutowa mayowe ya kuzomeya baada ya kunyimwa fursa ya kuzungumza.

Mwandishi : Mohamed Dahman /AFP

Mhariri : Josephat Charo