1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wole Soyinka-mshindi wa zawadi ya amani ya Nobel ya uandishi fasihi aliingilia jukwaa la kisiasa nchini mwake

Oumilkher Hamidou27 Septemba 2010

Muanadishi vitabu mashuhuri wa Nigeria aamua kujibwaga katika jukwaa la akisiasa kwa lengo la kutetea masilahi jumla ya nchi yake Nigeria

https://p.dw.com/p/PNtw
Wafaanyakazi katika kisima cha mafuta cha Niger Delta nchini NigeriaPicha: picture-alliance/dpa/dpaweb

Mshindi wa zawadi ya amani ya Nobel,muandishi vitabu Wole Soyinka wa Nigeria ameamua kujishughulisha na siasa nchini mwake.Jumamosi iliyopita Wole Soyinka amekabidhiwa wadhifa wa chama alichokiunda mwenyewe cha kisiasa.Hata kama chama hicho kinaotea kuiona Nigeria ikiongozwa na watu waliotakasika na rushwa,wadadisi hawaamini lakini kama chama hicho kitashinda katika uchaguzi wa bunge na rais hapo mwakani.

Chama hicho kwa jina "Muungano wa kidemokrasi kwaajili ya umma wa shirikisho-DFPF kimetokana na vuguvugu la maandamano wakati wa utawala wa muimla wa zamani Sani Abacha.Mwaka mmoja baada ya kutwaa madaraka mnamo mwaka 1993,Wole Soyinka alishitaki katika mahakama kuu ya mjini Lagos kutaka utawala wa Abacha utangazwe kuwa haramu.Kesi yake ilishindwa na Soyinka akakimbilia nchi za nje na kusaidia kuunda vuguvugu la wapinzani wa Abacha uhamishoni.Baada ya kifo cha Abacha mwaka 1998 vuguvugu hilo likaendelea na harakati zake kupigania usawa na kuwapiga vita wala rushwa.Baada ya majaribio kadhaa,mwaka huu chama cha DFPF kimefanikiwa kuandikishwa kupigania uchaguzi.Na Wole Soyinka pia ni miongoni mwa wagombea:

"Lengo la chama sio kushinda uchaguzi wa rais,bali kufanikiwa kuingia katika daraja za uongozi katika serikali za miji hadi kufikia majimbo.Kwasababu uchaguzi wa maeneo hayo ndio utakaoamua nani atakua rais mpya wa Nigeria."

Zaidi ya vyama 60 vimeruhusiwa hadi sasa kujiandikisha katika uchaguzi huo.Upande wa upinzani nchini Nigeria umegawika.Ndio maana chama cha DFPF,hakina nafasi nzuri ya kushinda,hata kama Wole Soyinka anakiongoza.Hayo ni kwa mujibu wa Klaus Pähler anaeaongoza ofisi ya wakfu wa Konrad Adenauer mjini Abuja.Anaamini katika uchaguzi wa mwakani pia mojawapo ya makundi matatu ya kikabila ndio yatakayoamua na sio masilahi jumla.

"Unaona unapofuatilizia Blogi katika mtandao,watu wanasema Soyinka ni wa kabila la Yoruba kwa hivyo hawezi kukubaliwa na wa Igbos.Watu wanaosoma vitabu hapa na ambao pengine wanamjua mshindi huyo wa zawadi ya amani ya Nobel na kuyatambua malengo yake,ni kidogo sana."

Hata hivyo wengi wa wakaazi wa Nigeria wanaotea kuona utajiri wa nchi hiyo haumalizikii mifukoni mwa baadhi tu ya viongozi.Hata Soyinka mwenyewe anaungama kwamba watu wa hirimu yake wamewavunja moyo wananchi wa Nigeria.Pengine hii ikawa fursa ya mwisho kwa mwandishi vitabu huyo mwenye umri wa miaka 76 kuweza kuibadilisha nchi yake.

Mwandishi: Adrian Kriesch/ZR/hamidou,Oummilkheir

Mpitiaji:Mohammed Abdul-Rahman