1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wolfsburg yaachana na kocha Hecking

Sekione Kitojo
18 Oktoba 2016

Klabu ya soka ya Wolfsburg imeachana na kocha wake Dieter Hecking Jumatatu(17.10.2016) baada ya matokeo mabaya mwanzoni mwa msimu wa Bundesliga,ambapo timu hiyo ina pointi sita kutokana na michezo saba.

https://p.dw.com/p/2RNL4
Deutschland VfL Wolfsburg - RB Leipzig
Picha: Getty Images/Bongarts/S. Franklin

Klabu hiyo  imesema  uamuzi  huo  umefikiwa , kwa "makubaliano  maalum" kufuatia  mkutano  baina  ya  Hecking  na  mkurugenzi  wa  spoti  Klaus  Allofs.
Hecking  ameshindwa  kupata  uungwaji  mkono  wowote  kutoka  kwa  Allofs kufuatia  kipigo  siku  ya  Jumapili  cha  bao 1-0 nyumbani  dhidi  ya  timu  iliyopanda  daraja  ya  RB Leipzig.

Valerien Ismail , kocha  wa  kikosi  cha  wachezaji  wa  akiba  wa  Wolfsburg , atachukua  hatamu  za  kuifunza  timu  hiyo kwa  muda, klabu  hiyo  imesema. Ismail ni  mchezaji  wa  zamani  wa  Werder  Bremen na  Bayern  Munich  akiwa  mlinzi.

Deutschland VfL Wolfsburg - RB Leipzig
Wachezaji wa Wolfsburg wakiwa wamekata tamaa baada ya kufungwa baoPicha: Getty Images/Bongarts/S. Franklin

Wolfsburg  ilianza  msimu  huu  ikiwa  na  kikosi  kilichofanyiwa  mabadiliko  na  kuwa  na  matumaini  ya  kufikia  katika  mashindano  ya  Ulaya. Lakini  klabu hiyo  iko  katika  nafasi  ya  14  baada  ya  michezo saba  licha  ya  kumpata  mchezaji  wa  kimataifa  wa  Ujerumani Mario Gomez.
"Licha  ya  kucheza  vizuri  katika  Champions League , tumeshindwa kufanikiwa  kufuzu katika  mashindano  ya  kimataifa ya  Ulaya," Allofs  alisema  katika  taarifa. "Na  mabadiliko  ya  kikosi  hayakuleta matokeo tuliyotarajia.

"Baada ya  matokeo  ya  hivi  karibuni  ya  kuvunja  moyo, tumeamua kuipa  timu msukumo  mpya kwa  kumbadilisha  kocha,Allofs  alisema. Hecking amesema , amekatishwa  tamaa."

Wolfsburg Fußballer Mario Gomez (M)
Dieter Hecking (kushoto) , Mario Gomez (katikati) na Klaus Allofs (kulia)Picha: picture-alliance/dpa/J. Stratenschulte

Hecking amekuwa  kocha  wa  Wolfsburg  muda  mfupi  kabla  ya  Krismass  mwaka  2012. Mwaka  2015, Wolfsburg  ilishinda  kombe  la  Ujerumani  na  kumaliza  ikiwa  ya  pili  kwa  Bayern  katika  Bundesliga, ikipata  ushindi  wa  mabao 4-1  dhidi  ya  mabingwa  hao. Ilifikia  robo  fainali  ya  Champions League  msimu  uliopita, ikishindwa  na  waliokuja  kuwa  mabingwa  Real Madrid. Hecking  ni kocha  wa  tatu  katika  Bundesliga  kupoteza  kazi  yake msimu  huu , baada  ya  kocha  wa  Werder  Bremen Viktor Skripnik  na  Bruno  Labbadia  wa  hamburg.