1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wsaudi 27 na mgeni 1

23 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CfVj

RIYADH:

Polisi ya Saudi Arabia ambayo ilitangaza kuwakamata watu 28 kwa tuhuma za kuandaa njama ya kuhujumu vituo vitakatifu vya kiislamu kandoni mwa miji ya Mecca na Medina wakati wa hija ya majuzi ,imearifu kuwa 27 kati yao ni wasaudi na mmoja ni raia wa kigeni.

Tangazo hilo limetolewa siku 2 baada ya wizara ya ndani ya Saudia kusema imewatia nguvuni watu kadhaa na kufuja njama ya kuhujumu vituo vitakatifu nje ya Mecca na Medina.